SABASABA 2018

Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akimsikiliza Mkaguzi wa Polisi (INSP) Alex wa Kikosi cha Kutuliza ghasia makao makuu akielezea namna shughuli mbalimbali za kikosi hicho ikiwemo kutuliza ghasia.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Barnabas Mwakalukwa (kulia) akimuonesha Kamishna wa Polisi jamii (CP) Mussa .A. Mussa baadhi ya vipeperushi vya Jeshi la Polisi vinavyotumika katika utoaji wa elimu kwenye banda la Polisi, viwanja vya Sabasaba.

Kamishna wa Polisi jamii (CP) Mussa A. Mussa akimsikiza askari wa Usalama barabarani CPL Faustina katika banda la Jeshi la Polisi wakati wa maonesho ya 42 ya biashara ya kimataifa.