KAMANDA WA KIKOSI

ACP PAULO KASABAGO

 

KITENGO CHA KINYWA
Kitengo hiki kipo mbioni kuboresha huduma zake za mano na kinywa katika nyanja zifuatazo:-

 • Kung’oa meno yalioota vibaya (Disimpaction).
 • Kung'oa meno
 • Kuuwa kiini cha jino (Root canal treatment)
 • Kusafisha meno (Scalling & root canal).
 • Kerekebisha meno yaliokaa vibaya
 • Upasuaji mdogo (Minor surgery)

Ni kitengo kinachoongozwa na Dr. Risala (DO/DS). Tunahitaji wafadhili mbalimbali watakaokuwa tayari kutupatia vifaa vya tiba ya Kinywa na Meno.

Kitengo Cha Kinywa

Daktari Msaidizi wa kinywa na Meno (ADO), Dr Alibariki (Mkaguzi msaidizi wa Polisi) akitoa huduma ya kinywa na meno katika hospitali ya Kilwa Road, Dar-es-salam. Pembeni yake akisaidiwa na WP Bett. Kwa sasa kitengo cha meno kinatoa huduma ya kung’oa meno na ushauri kuhusu afya ya kinywa na meno kutokana na uhaba wa vifaa

KITENGO CHA TB

Kitengo cha TB katika Hospitali ya Kilwa Road kinaongozwa na mkaguzi Dr. Mariam na kinahusika na wagonjwa wa TB na Ukoma. Wagonjwa wa TB, HIV/AIDS na ukoma wanapofikika katika hospitali ya Kilwa road, kwanza hufanyiwa mchujo wa kutambua dalili za magonjwa husika kwa kuulizwa maswali maalum ambayo humpelekea daktari kumshauri mgonjwa ni vipimo gani atahitaji kupima uli kupata uhakika wa tatizo husika la mgonjwa. Maswali hayo ni muongozo wa awali wa kutambua aina ya tatizo la mgonjwa.
Mgonjwa anapopimwa na kugundulika tatizo lake huanza kutumia dawa za magonjwa. Dawa za TB na HIV zinatolewa bure kwa wagojwa wote. Ugonjwa wa TB unatibika na kama tunawagojwa wetu tuwashauri wafike kituo chochote cha kwa ushauri na mataibabu.

Kitengo Cha TB

WP Sgt Sophia akimsikiliza mgonjwa katika  kitengo cha TB katika hospitali ya Kilwa Road.

 KITENGO CHA ULTRA SOUND

Dr. Gaspa Kiluvya

Dr. Gaspa Kiluvya

Dr. Gaspa Kiluvya, Mtaalam wa ultra sound na mkuu wa kitengo cha Ultra sound katika Hospitali ya Kilwa Road Dar-es-salaam akimpatia maelezo mgonjwa wake juu ya huduma ya Ultra sound. Hospitali ya Kilwa Road inatoa huduma ya Ultra sound kwa askari na raia kuanzia saa 2.30 asubuhi hadi saa 9.30 alasiri kila siku jumatatu hadi ijumaa.

KITENGO CHA UKUNGA

Hospitali ya Kilwa road kwa sasa ina wodi nzuri na wataalam na wenye uzoefu wa kutosha katika fani ya ukunga. Tunao wataalam wa upasuaji na chumba cha upasuaji(theater) kwa wale wazazi ambao uzazi wao utahitaji upasuaji. Kadi za Bima ya Afya zinatumika kwa wagojwa wa aina zote. Wodi ya wazazi inafanya kazi masaa 24 na ipo wazi kwa siku zote kuanzia jumatatu hadi jumapili. Ewe askari na raia, unasubiri nini kumpeleka mke wako akajifungulie katika Hospitali ya Kilwa Road?. Mgonjwa anapolazimika kupelekwa katika hospitali ya rufaa, gari la wagonjwa la uhakika
(ambulance) linapatikana masaa 24. Karibu upate huduma bora ili uwataarifu na wengine.

Cpl Merecy,WP Dodatha na Angela Komba

 Wa kwanza kulia ni Cpl Merecy, katikati ni WP Dodatha na wa wisho ni Angela Komba, wote kwa pamoja ni wakunga katika kitengo cha ukunga.

KITENGO CHA MAABARA

KITENGO CHA MAABARA KITENGO CHA MAABARA

KITENGO CHA MAABARA KITENGO CHA MAABARA

Ni maabara ya Kisasa iliosheheni vifaa vya kutosha na wataalam waliobobea   katika fani ya maabara. Idara hii inaoongozwa na ASP Simon Lutengano Wakachu [Health laboratory Technologist} akishirikiana na Mkaguzi wa Polisi Isaya Lameck Ndimila [Health Laboratory Scientist and Biochemistry Specialist} Hatuna budi kuwashukuru wafadhili wetu watu wa marekani kupitia   Pharm Access International na MUHAS kwa kutupatatia vifaa hivi vya kisasa vya maabara. Huduma nyingi zinapatika katika maabara ya Hospitali ya Kilwa Road, Hii ikiwa ni pamoja na Vipimo vyote vya Parasitology & Entomology (BS, stool and urine analysis), Hematology and Blood transfusion (FBP, ESR, HB, Blood Group, Sickling Test), Microbiology (Widal Test, UDRL, Urine for Pregnant, Gram Stain) and TB & Leprosy  (Sputum for AFB, Skin smear,  CD4 count nakazalika). Vipimo vya    chemistry kama vile figo moyo mafuta na kazalika na watalam hawa pamoja na kufanya uchunguzi wa vimelea mbalimbali vya magonjwa bado wanalojukumu la kufundisha wanafunzi gazi ya cheti kwa fani ya maabara kwa mwaka mmoja.

KITENGO CHA UPIMAJI NA USHAURI NASAHA

KITENGO CHA UPIMAJI NA USHAURI NASAHA

 S/SGT Asia akimkabidhi dawa mgonjwa katika kitengo cha Upimaji wa hiari na Ushauri nasaha (CTC/VCT) katika hospitali ya Kilwa Road Dar-es-salaam. Pembeni yake ni WP Mary
Waathirika na wagonjwa wa VVU (HIV/AIDS) wanapatiwa vipimo, ushauri nasaha na wanapogundulika wameathirika na VVU wanapatiwa dawa za kupunguza makali ya VVU. Huduma hii ni bure kwa watu wote. Kazi zinazofanywa na idara hii ni pamoja na :-
Kutoa ushauri wa kupima afya kwa hiari.
Kuagiza na kutoa dawa za kupunguza makali ya VVU.
Kusajili wagonjwa wasioanza nawanaoanza dawa za kupunguza akali ya VVU.
Kutoa ushauri wa lishe kwa wagonjwa.
UKIMWI upo na endapo utafuata masharti ya wataalamu na matumizi sahihi ya dawa, utaishi muda mrefu na hutajihisi kama wewe ni mgonjwa. Karibu Kilwa Road Hospitali na karibu kwenye huduma.

 STOO KUU YA DAWA

Cpl James na WP Neema

Cpl James na WP Neema wakiwa katika stoo kuu ya dawa

Kilwa Road hospitali kwa sasa ina dawa za kutosha inazonunua toka MSD. Mgonjwa anapoandikiwa dawa za matibabu hatarajii kupata usumbufu wowote wa dawa kwa wale wagonjwa wa Bima na wasio na Bima. Mgonjwa anatakiwa kufahamu kuwa si dawa zote zinapatikana kupitia huduma ya Bima, Kuna baadhi ya dawa hazipo katika huduma ya Bima, hivyo mgonjwa anapaswa kununua dawa hizo. Jengo la stoo kubwa ya dawa katika hospitali ya Kilwa road lipo katika hatua ya mwisho ya umaliziaji

  KITENGO CHA UZAZI NA KLINIKI YA WATOTO

Mkuu wa Kitengo cha wazazi na kliniki ya watoto (RCH)

 CPL HAPPY

Idara hii inahusika na kazi zifuatazo:-

 • Upimaji wa uzito wa watoto ili kufahamu maendeleo yao.
 • Kuwapima wamama wajawazito na kufuatilia maendeleo ya afya zao.
 • Kutoa chanjo kwa watoto na wajawazito.
 • Kupima VVU kwa wakina mama pamoja na wenzi wao na kuwapa dawa za kinga kwa wamama wajawazito walioathirika naVVU.
 • Kuwapima watoto waliozaliwa na kina mama walioathirika na VVU kama wamepata maambukizi.
 • Kutoa huduma ya uzazi wa mpango kwa wakina mama.

Huduma hizi zinapatikana kila siku katika hospitali ya Kilwa road kuanzia jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa 2.30 asubuhi hadi saa 9.30 alasiri.

  WODI

WP Stella-Wodini

WP Stella akimpima mgonjwa Presha alielazwa katika wodi ya wanaume ya Hospitali ya Kilwa Road.


Hospitali ya Kilwa road ina wodi nzuri na safi kwa wakati wote, Tunao wauguzi wa kutosha katika wodi zetu na vitanda vya kutosha kwa jinsia zote na rika zote. Huduma ya kulaza wagonjwa inapatikana masaa 24 kila siku. Wodi zetu zipo karibu kabisa na barabara ya Kilwa. Upo mgahawa wa kisasa kabisa karibu na wodi kwa ajili ya wafanyakazi, jamii inayotuzunguka na wagonjwa wetu kupata huduma za chakula na vinywaji.

CHUMBA CHA UPASUAJI

Kitengo cha upasuaji (thearter) kinafanya upasuaji mkubwa na upasuaji mdogo.
Upasuaji mkubwa ni pamoja na:-

 • Wanawake wenye matatizo ya uvimbe tumboni ndani ya kizazi au nje ya kizazi.
 • Uvimbe uliojaa maji kwenye mifereji ya mayai ya kike
 • Shingo ya uzazi kutoka nje
 • Kidole tumbo
 • Upasuaji wa mzazi wenye tatizo la kujifungua.
 • Upasuaji wa henia

Na upasuaji mdogo ni pamoja na:-

 • Kushona majeraha
 • Kupasua majipu.
 • Kutairi
 • Uvimbe mdogo mdogo wa maji.
 • Uvimbe wa mafuta unaojikusanya sehemu moja mwilini

 KITENGO CHA MIPINGO NA UTAFITI

Cpl Flora Katunz

Cpl Flora Katunzi,  akiwa katika Ofisi yake ya Mipango na Utafiti eneo la Kilwa Road Hospitali ,Pia ni mtaalam wa jinsia

Kikosi cha Afya kina kitengo/idara ya Mipango na Utafiti. Idara hii inahusika na :-

 • Kuandaa mipango ya muda mrefu na muda mfupi ya kikosi cha Afya.
 • Kukishauri kikosi katika mambo ya kimaendeleo.
 • Kuandaa taarifa mbalimbali za kikosi.
 • Kuandaa tafiti mbalimbali za kikosi.
 • Kuhifadhi takwimu za kiutendaji za kikosi.
 • Kuandaa taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kikosi cha Afya