ACP MBOJE J.S KANGA

ACP MBOJE J.S KANGA

Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji Tanzania

SSP AHMED A. KINYUNYU

SSP AHMED A. KINYUNYU
Afisa Mnadhimu Mkuu wa Polisi Kituo cha Wanamaji Dar es Salaam

SSP VENANCE M. KAZIMILI

SSP VENANCE M. KAZIMILI

SP.WENCESLAUS A. NYANTORA

SP.WENCESLAUS A. NYANTORA
Mkuu wa Kituo cha Wanamaji Dar es Salaam (OCS)

KAZI ZINAZOFANYWA NA KIKOSI CHA WANAMAJI

Kazi za Kikosi cha Wanamaji zimeainishwa kwenye PGO. 13 (2) (a-d) ambazo ni:-

 1. Kufanya doria kwenye maji ya bahari na maziwani(Territoraial and inland waters)
 2. Kusaidia operesheni za vikosi vingine vya Polisi kwenye maji
 3. Kufanya kazi ya utafutaji na uokoaji kwenye maji
 4. Kulinda mali za serikali kwenye maji

Pamoja na hizo kazi tunafaya pia kazi zifuatazo:-

 1. Kuzuia kazi za uvuvi haramu hasa uvuvi wa baruti
 2. Kuzuia uharibifu wa mazingira kwenye maji
 3. Kupambana na wahamiaji haramu, wakwepa ushuru na wanaosafirisha mazao ya misitu kinyume cha sheria majini
 4. Kupambana na uharamia na kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria

Maafisa wa Polisi wakiongozwa na aliyekuwa RPC Mwanza SACP Simon Siro

Maafisa wa Polisi wakiongozwa na aliyekuwa RPC Mwanza SACP Simon Siro akiwa na maafisa wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa, wakufunzi kutoka Marekani, Maafisa wa Ubalozi wa Marekani na wageni mbalimbali walioalikwa kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kwanza kwenye Chuo cha Wanamaji Mwanza mwaka 2011

Majengo ya Chuo cha Wanamaji

Majengo ya Chuo cha Wanamaji ya awamu ya kwanza ambayo yalitumika kwa ajili ya kozi ya Maritime Interdiction of Terrorism, Mwanza.

mafunzo ya kuzuia ugaidi  mafunzo ya kuzuia ugaidi

Askari wa Polisi Wanamaji wakiwa kwenye mafunzo ya kuzuia ugaidi (Comprehensive Maritime Security Manda Bay, Kenya). Mafunzo haya yanatolewa na serikali ya Marekani kuwajengea uwezo Askari na baadaye kuwa wakufunzi wa wengine. Mafunzo yanayotolewa ni:-

 • Comprehensive Maritime Security
 • Maritime Port and Harbors Security
 • Advanced Outboard Motor Maintenance
 • Maritime Interdiction of Terrorism

Kikosi cha Polisi Wanamaji Kina seksheni nne ambazo ni:-

 • Nahodha (Navigation)
 • Ufundi (Engineering)
 • Uzamiaji ( Scuba diving)
 • Ubaharia (Seamanship)

Nahodha D.5815 S/SGT Maximillian   Nahodha D.5815 S/SGT Maximillian

Nahodha D.5815 S/SGT Maximillian akiwa katika shughuli ya kuongoza meli wakati wa doria ndani ya Bot PB. 20 Mamba.

Fundi A/INSP Bakari   Fundi A/INSP Bakari

Fundi A/INSP Bakari Fumbwe akirekebisha mitambo wakati wa doria kwenye Boti PB. 20 Mamba

 Boti mpya Fibre glass PB.21

Boti mpya Fibre glass PB.21 Ulinzi Shirikishi ikiwa kwenye ghati tayari kwa doria. Boti hii hufanya doria Territorial waters

Boti PB. 20 Mamba

Boti PB. 20 Mamba ikiwa kwenye ghati. Boti hii hutumika kwa doria kwenye Territorial waters.

Mashua 2 za Fibre Glass tulizopewa na Serikali ya Marekan

Mashua 2 za Fibre Glass tulizopewa na Serikali ya Marekani ambazo zitafanya kazi ya kuzuia uhalifu kwenye mwambao wa bahari ya Hindi. Boti hizi ziko saba na zimegawiwa kama ifuatavyo:-

 • Mwanza – 2
 • Dar es Salaam – 2
 • Zanzibar – 2
 • Tanga – 1

Kwa vile nia ya Kikosi ni kukifanya kiwe cha kisasa kwa kutumia teknolojia za kisasa, tumekuwa tukitoka taratibu kwenye teknolojia ya zamani na kuanza kutumia Computer kwa ajili ya utunzaji kumbukumbu za askari na sasa tuna data base ya askari wote wa Polisi Wanamaji Tanzania.

Insp Naanjela

INSP Naanjela – Mtaalamu wa IT akiwa kazini

Penina Ndembo

Katibu Muhtasi Ndugu Penina Ndembo akiwa kazini

JOSEPH O ABACH

NDUGU JOSEPH O ABACH
Mhasibu wa Kikosi Ndugu Joseph O. Abach ambaye hushughulikia mambo yote yahusuyo fedha.

ASP MOHAMED

Kikosi hiki kina Idara pia ya Intellijensia ambayo inaongozwa na ASP Mohamed. Kazi kubwa ni kukusanya taarifa za kiitelijensia na kuzitumia wakati wa kufanya doria. Doria hizi zinatakiwa kuwa zenye malengo.

Kikosi cha Wnamaji Tanzania ndicho hushughulikia vituo vingine vya Wanamaji kwenye mambo ya kiufundi. Askari NO. E.7216 P.C Deogratias Mihanda ndiye mtunza stoo ya kikosi, huingiza na kutoa vifaa vyote ambavyo vinatakiwa mikoani.

Ajira katika Kikosi cha Polisi Wanamaji wanatakiwa wawe na ufahamu wa maeneo yafuatayo:

 • Ubaharia na upigaji mizinga (seamanship and gunnery)
 • Unahodha (Navigation)
 • Ufundi wa meli (Marine Engineering)
 • Uzamiaji (Scuba diving)
 • Umeme (Electrician)
 • Utaalamu wa Rada (Radar technicians)
 • Utaalamu wa kutuma Rada (Radar Operations)
 • Upakaji rangi wa meli (Painting)
 • Upishi (Catering)